Kanali afungwa jela miaka 21 Rwanda

Aliyekuwa kamanda mkuu wa kikosi cha ulinzi wa Rais Paul Kagame, Kanali Tom Byabagamba, amehukumiwa kifungo cha miaka 21 jela na kuvul...


Aliyekuwa kamanda mkuu wa kikosi cha ulinzi wa Rais Paul Kagame, Kanali Tom Byabagamba, amehukumiwa kifungo cha miaka 21 jela na kuvuliwa cheo chake baada ya kupatikana na hatia ya kuharibia sifa nchi hiyo na kuhamasisha wananchi kupinga utawala.
Kesi hiyo ilimhusisha pia jenerali mstaafu Frank Rusagara ambaye naye amepatikana na hatia na kuhukumiwa miaka 20 jela.
Maafisa hao wa jeshi wamepinga hukumu hiyo wakisema mashtaka dhidi yao yalichochewa kisiasa.
Mahakama imeunga mkono hoja za upande wa mwendesha mashtaka kwamba mlinzi wa muda mrefu wa Rais Kagame, Kanali Byabagamba, alihusika na makosa matatu ambayo ni kueneza kampeni za chuki dhidi ya utawala ambazo zingesababisha wananchi kugoma dhidi ya serikali ya nchi hiyo na kutoheshimu bendera ya nchi hiyo.
Jenerali mstaafu Frank Rusagara naye amepatikana na makosa kama hayo pamoja na kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria.
Awali alikiri kumiliki bastola mbili alizopewa kama zawadi na nchi za Afrika Kusini na Israel, wakati alipokuwa afisa mkuu anayehusika na ununuzi wa silaha katika wizara ya ulinzi ya Rwanda.
Maafisa hao wamekata rufaa baada ya mahakama kutangaza hukumu hiyo.

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item