Doukara apigwa marufuku ya mechi nane
Mshambuliaji wa klabu ya Leeds United Souleymane Doukara, amepigwa marufuku ya mechi nane kwa kumng'ata mchezaji mwingine. Mchezaj...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/03/doukara-apigwa-marufuku-ya-mechi-nane.html
Mshambuliaji wa klabu ya Leeds United Souleymane Doukara, amepigwa marufuku ya mechi nane kwa kumng'ata mchezaji mwingine.
Mchezaji
huyo wa umri wa miaka 24 analaumiwa kwa kusababisha timu yake kutoka
sare ya bao moja na Fulham mnano tarehe 23 mwezi Februari.Doukara ambaye alipinga hatua hiyo pia amepigwa faini ya dola 5000.
Leeds United imekasirishwa na matokeo ya kisa hicho pamoja na urefu wa hukumu lakini imesema haitatoa taarifa zaidi kwa sasa.
Marufuku hiyo inamaanisha kuwa hatashirika kandanda hadi wakati mechi ya mwisho ya msimu.