MAMBO MATANO YA KUISAIDIA NIGERIA BAADA YA KUSHINDWA KUFUZU AFCON 2017

Kwa mara nyingine Nigeria Super Eagles watakosekana  kwenye michuano ya mataifa ya Afrika (African Nations Cup) kwa mara ya pili mfululiz...

Kwa mara nyingine Nigeria Super Eagles watakosekana  kwenye michuano ya mataifa ya Afrika (African Nations Cup) kwa mara ya pili mfululizo baada ya kukubali kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa Misri kwenye mchezo wa marudiano na kufanya matokeo ya jumla kuwa 2-1baada ya kucheza michezo yote miwili.
Kwan nchi yenye wakazi wengi kuliku nchi nyingine za kiafrika, ambayo inatoa wachezaji wengi kwenda nje ya Afrika na imekuwa juu ya soka la Afrika kwa muda mrefu ni jambo la kushangaza kushuhudia Nigeria ikianguka.
Kushindwa kufuzu kwa msimu huu kunaifanya kuyakosa mashindano hayo kwa mara tatu ndani ya miaka minne. Hiyo inaonesha kwamba Nigeria imekuwa kama chambo na kutokana na kiwango wanachokionesha wanatakiwa kuangaliwa kama chambo kwenye soka la Afrika.
Kutambua tatizo ni hatua ya kwanza kuelekea kutauta ufumbuzi, na hapa ndipo Nigeria wanahitaji kuanzia:
  1. Kumwacha Samson Siasia aendelee kuwa kocha mkuu
Wakati matatizo yanaanza kwenye kikosi cha Nigeria, ilijikuta kikaangoni pale iliposhindwa kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2012.
Badala ya kurudi nyuma kuangalia kwanini timu ilishindwa kufuzu na kipi kilihitajika kufanywalakini haraka Siasia alitimuliwa kazi. Licha ya kwamba kikosi cha wakati huo kilikuwa kikicheza soka la kuvutia, kilikua pia kinafunga magoli ya kutosha.
Kipindi hiki cha kutafuta nafasi ya kufuzu kwa michuano ijayo, makocha watatu wakiwa na style zao tofauti za ufundishaji na wamewaita wachezaji tofautitofauti kila mmoja kwa kipindi chake. Kila kocha akija na nahodha wake tofauti.
Siasia ameteuliwa kama kocha wa muda, lakini ni wakati sahihi chama cha soka cha Nigeria (NFF) kumpa mkataba wa muda mrefu kuendeleza harakati alizozianza.
Hakuna haja ya kocha mpya kuja tena na kuanza upya kwenye mchakato ambao tayari umeanza kupamba moto.
Tulichokiona kwenye dakika zaidi ya 180 dhidi ya Misri ni wachezaji kucheza soka safi kitimu, kutengeneza nafasi, na kikaonesha kuwa kitakuwa vizuri baada ya muda lakini kinaangushwa na safu ya ulinzi.
Wapewe muda na kwa msaada wa kiufundi wanaoupata kutoka kwa Shaibu Amodu hii ni timu ambayo inaweza ikafika mbali kama wataamua kumpa muda kocha.
  1. Soka lazima liwe huru
Ni rahisi kutupa lawama zote kwa NFF, kiungwana hiki ndiyo chombo ambacho kinasimamia soka hivyo kinatakiwa kuwajibika. Nigeria imeshindwa kufuzu chini ya uongozi wa makocha watatu tofauti ni kitu cha kushangaza.
Serikali kuingilia shughuli za NFF inaweza ikawa sababu ya kushindwa kufanya kazi zake vizuri. Kusubiri kwa miezi kadhaa kuhusu masuala ya kifedha kukamilishwa hata baada ya bajeti kuwa iko wazi hii inaiathiri timu kwenye maandalizi na mipango yake
  1. Wachezaji lazima waoneshe utayari wao
Siku za nyuma wakati Nigeria ikiwa ni timu tishio barani Afrika, wachezaji wake hawakuwa wakicheza kwenye vilabu vikubwa vya Ulaya. Na wakati huo kunawachezaji walikuwa hawana timu, walichokuwa wanakifanya ni kujitoa na kupambana kwa ajili ya timu yao.
Na timu ya kipindi hicho ndiyo iliitambulisha The Super Eagles nje ya mipaka ya Afrika. Wakati huo wachezaji walikuwa na uzalendo na kujiamini na walikuwa wakionekana hivyo katikati ya uwanja.
Nigeria ilimtunza kocha na kumwachia majukumu ya kuijenga tofauti na sasa ambapo wachezaji wamekuwa hawana uhakika kama wataitwa kwenye mechi inayofuata au la.
  1. Kutengeneza mfumo utakaombeba Ighalo
Kwasasa striker wa Watford Odion Ighalo bila shaka ndiye mchezaji hatari zaidi barani Ulaya. Ameweza kufunga magoli ya kutosha kwenye Premier League lakini akiwa na Nigeria ameshindwa kufunga hata goli moja kwenye michezo miwili na hapa ndipo maswali yanaweza kuibuka. Je watu watilie mashaka kiwango chake? Au mfumo haumfanyi ang’ae?
Ushahidi ambao mtu anaweza kutoa kutokana na michezo hiyo miwili ni kwamba, mfumo ndiyo tatizo. Kwa kipindi kirefu, Ighalo alionekana pekeake akiwa katikati ya mabeki wawili akiwa hana msaada. Kuna wakati alishuka chini na kuchukua mpira akaenda pembeni kisha akampigia pasi Ahmed Musa ambaye alikuwa amesogea katikati ya uwanja lakini alishindwa kuusoma mchezo huo na hakuukimbilia mpira.
Alicheza vizuri baada ya Alex Iwobi kuingia, kinda wa Arsenal mwenye uwezo wa kukimbia na walikuwa wakibadilisha nafasi hali iliyowapa shida mabeki wa Misri
Ni wakati muafaka sasa kwa Siasia kubadilisha mfumo ili uwafit wachezaji anaowatumia. Mashabiki wengi tayari wameanza kumkosoa Ighalo na litakuwa kosa kubwa kwa Siasia kumtema mchezaji huo.
Rashidi Yekini alipoteza nafasi kibao, lakini anajiamini kwasababu anajua kwamba kocha na wachezaji wenzake wanaimani nae. Jambo hili pia Ighalo anahitaji kuwanalo.
  1. Marekebisho kwenye safu ya ulinzi
Eneo la ulinzi lilitumika kama sehemu muhimu ya kikosi cha Nigeria. Lakini miaka ya hivi karibuni kitu hicho hakipo kwenye kikosi hicho. Stephen Keshi alijitahidi kuliziba pengo hilo kwa kucheza style ya kuzuia ambayo ilikuwa haipendezi kuangalia japo ilimsaidia lakini bado sehemu hiyo haijawa salama kwa muda sasa.
Siasia amekuwa na mfumo wa aina nyingine wa kushambulia. Ukifanikiwa ni mfumo unaovutia lakini timu ikishindwa kufunga unakuwa hatari.

Related

MICHEZO 3141533199863188379

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item