Blackwell: Sitapigana tena
Nick Blackwell amesema kuwa hatapigana tena baada ya kupata majeraha mabaya ya kichwa katika pambano la kutetea taji lake la uzani wa...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/04/blackwell-sitapigana-tena.html
Nick Blackwell amesema kuwa
hatapigana tena baada ya kupata majeraha mabaya ya kichwa katika pambano
la kutetea taji lake la uzani wa kati nchii Uingereza kwa Chris Eubank
Jr.
Blackwell mwenye umri wa miaka 25,alikosa fahamu baada ya
kuvuja damu katika fuvu lake la kichwa baada ya kupoteza pigano hilo
katika raundi ya kumi katika ukumbi wa Wembley mnamo mwezi Machi 26.''Sitopigana tena'',raia huyo wa Uingereza alituma ujumbe wake katika mtandao wa twitter alipoulizwa iwapo atarudi katika masumbwi.
''Siwezi kuwaweka marafiki zangu,na ndugu zangu katika hali kama hiyo tena''.
Blackwell anataka kuendelea na masumbwi katika kiwango fulani na anasema hana hisia zozote mbaya dhidi ya Eubank Jr wakati anapoendelea kuuguza majeraha.