Ghasia: Maduka ya raia wa Rwanda yaporwa Zambia
Ramani ya Zambia Zaidi ya watu 200 wamekamatwa katika mji mkuu wa Zambia Lusaka huku maandamano ya ghasia na wizi ukie...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/04/ghasia-maduka-ya-raia-wa-rwanda-yaporwa.html
![]() |
Ramani ya Zambia |
Zaidi ya watu 200 wamekamatwa katika
mji mkuu wa Zambia Lusaka huku maandamano ya ghasia na wizi ukiendelea
kwa siku ya pili mfululizo.
Makumi ya maduka yanayomilikiwa na
raia wa Rwanda yameporwa kufuatia madai kwamba raia wa Rwanda wamekuwa
wakishiriki katika mauaji ya kishirikina.Takriban watu saba wameuawa katika wiki za hivi karibuni na viungo vyao vya mwili kukatwa.
Inadaiwa kwamba viungo hivyo hutumika kufanyia uchawi.
Kuna zaidi ya wakimbizi 7000 wa Rwanda nchini Zambia.
Wengi wao wamedaiwa kutoroka maduka yao na makaazi
CHANZO,BBC