IS ladai kutekeleza shambulio la kwanza Somalia

Kundi la wapiganaji wa Islamic State limekiri kutekeleza shambulio lake la kwanza nchini Somalia. Linasema kuwa wapiganaji wake walileng...

Kundi la wapiganaji wa Islamic State limekiri kutekeleza shambulio lake la kwanza nchini Somalia.
Linasema kuwa wapiganaji wake walilenga vikosi vya Umoja wa Afrika katika shambulio la bomu mjini Mogadishu.
Islamic State limejaribu kujiimarisha nchini Somalia lakini limeshindwa kutokana na uwepo wa kundi la Alshabab,likiwa mshirika wa kundi pinzani la Al-Qaeda.
Taarifa hiyo kutoka IS haikusema ni lini shambulio hilo lilitekelezwa ama iwapo kulikuwa na majereha yoyote.
Wakati huohuo serikali ya Somalia imesema kuwa imemkamata kamanda mmoja wa kundi la IS aliyetoroka katika kundi la Al-Shabab ambaye amekuwa akitafutwa.
Kundi la IS limekuwa likitafuta uungwaji mkono kutoka kwa makundi ya wapiganaji nchini Somali kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa lengo la kuchukua udhibiti wa eneo la Afrika mashariki.

Related

MATUKIO 3461176469140882543

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item