Juventus yatwaa taji la Serie A

Klabu ya Juventus imetwaa Ubingwa wa Serie A huko Italy kwa mara ya 5 mfululizo. Ushindi huo umekuja baada ya Timu ya Pili kwenye Ligi N...

Klabu ya Juventus imetwaa Ubingwa wa Serie A huko Italy kwa mara ya 5 mfululizo.
Ushindi huo umekuja baada ya Timu ya Pili kwenye Ligi Napoli kufungwa 1-0 na AS Roma huko Stadio Olimpico Jijini Rome.

Juve waliifunga Fiorentina Bao 2-1 na kuhitaji Pointi 1 tu ili kujihakikishia Ubingwa lakini kipigo cha cha Napoli kimehakikisha hawawezi tena kuikamata Juve huku Mechi zikibaki 3.
Juve sasa wana Pointi 85 wakifuatiwa na Napoli wenye Pointi 73 na AS Roma wana Pointi 71.
Kwa kutwaa Ubingwa Msimu huu, Juve walionyesha umahiri mkubwa kwani hapo Oktobo 28 walikuwa Nafasi ya 12 wakiwa Pointi 11 nyuma ya Vinara wa Serie A.

Lakini baada ya hapo, Juve walishinda Mechi 24 kati ya 25 za Ligi zilizofuatia na kutoka Sare 1.
Katika Mechi hiyo Bao la ushindi la AS Roma lilifungwa Dakika ya 89 na Radja Nainggolan kutokana na ushirikiano mwema wa Mkongwe Totti, Pjanic na Mohamed Salah.

Related

MICHEZO 3690425128998594948

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item