Lucy kibaki na mkewe wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2007
Mke wa kwanza wa rais Lucy Kibaki amefariki katika hospitali mmoja mjini London kwa ugonjwa usiojulikana.
Lucy
alipata umaarufu kwa kumchapa kofi mpiga picha mmoja mwaka 2005 wakati
alipovamia afisi za kituo kimoja cha habari mwaka 2005 akikasirishwa na
vile habari moja ilivyoandikwa.
Katika kumbukumbu ya kumuhenzi bi
Kibaki rais wa Kewnya Uhuru Kenyatta alimsifu kwa jukumu lake
kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi nchini Kenya. Image caption
Lucy Kibaki pamoja na aliyekuwa mke wa aliyekuwa
rais wa Marekani George Bush ,Laura Bush.Picha kwa niaba ya Getty Images
Bwana Kenyatta alimrithi mumewe bwana Kibaki ambaye alitawala kutoka mwaka 2002 hadi 2013.
Bi Kibaki aliyezaliwa mwaka 1940,alijiondoa katika maisha ya hadharani wakati wa mwisho wa utawala wa mumewe. Image caption
Lucy Kibaki na mumewe Mwai KIbaki wakiwapungia mkono
wafuasi wao mda mchache baada ya kibaki kuwasilisha stakhabadhi zake za
uchaguzi katika tume ya uchaguzi mwaka 2007.Picha ni kwa niaba ya Getty
images
Mara ya mwisho kuonekana hadharani ni mwezi Agosti mwaka 2010,wakati alipofurahishwa na kupatikana kwa katiba mpya. Image caption
Lucy Kibaki na mumewe aliyekuwa rais wa Kenya Mwai
Kibaki pamoja na mkewe marehemu Kijana Wamalwa wakati wa misa ya kifo
cha Wamalwa.Picha kwa niaba ya Getty Images
Bwana Kenyatta alisema kuwa alikuwa mgonjwa kwa
kipindi cha mwezi mmoja uliopita ambapo amekuwa akipata matibabu nchini
Kenya na Uingereza.Bi Kibaki ni mwalimu ambaye aliwacha kazi yake kabla
ya ndoa yake na kibaki mwaka 1962 ili kuwalea wanawe