Maandamano makubwa yatarajiwa Baghdad

Al-Sadr ana ushawishi mkubwa Iraq Maandamano makubwa yanatarajiwa kufanyika leo katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad. Hatua hiyo inatok...

Al-Sadr ana ushawishi mkubwa Iraq
Maandamano makubwa yanatarajiwa kufanyika leo katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad.
Hatua hiyo inatokana na mgogoro wa kisiasa unaoshuhudiwa nchini humo pamoja na kukosekana kwa mabadiliko katika sera ya taifa.
Maandamano hayo yaliyoitishwa na kiongozi mmoja wa madhehebu ya Kishia na ambaye ana ushawishi mkubwa Moqtada al-Sadr yanatokea wakati amabapo Bunge la Iraq linajaribu kupiga kura kuidhinisha baraza jipya la mawaziri baada ya uhasama ulioshuhudiwa kwa wiki tatu sasa.
Waziri mkuu, Haider al-Abadi, amelitaka baraza la mawaziri la sasa ambalo lilibuniwa chini ya vyama vidogo vidogo vya kisiasa, kuondolewa na baraza jingine jipya libuniwe lenye watu walio na ujuzi wa sheria, kama mojawepo ya vigezo vya mfumo wake mpya wa kuiletea nchi hiyo mageuzi yafaayo.
Mwaandishi wa BBC mjini Baghdad anasema kuwa huu ndio mgogoro mbaya sana wa kisiasa nchini Iraq tangu kuangushwa kwa utawala wa Saddam Hussein mnamo mwaka wa 2003.

Related

MATUKIO 3020286199747312809

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item