Mahakama yatupa 'sheria ya matusi' mtandaoni Keny

Jaji Ngugi amesema makosa yanayoangaziwa yanaweza kushughulikiwa na sheria nyingine Mahakama Kuu jijini Nairobi imeamua kwamba Kifung...

Jaji Ngugi amesema makosa yanayoangaziwa yanaweza kushughulikiwa na sheria nyingine
Mahakama Kuu jijini Nairobi imeamua kwamba Kifungu cha Sheria ambacho kimekuwa kikitumiwa kuwafungulia mashtaka watu kuhusiana na ujumbe kwenye simu na mitandao ya kijamii Kenya ni haramu.
Jaji wa Mumbi Ngugi alisema kifungu hicho, cha kutumia vibaya kifaa cha mawasiliano, kinakiuka katiba.
Kifungu hicho nambari 29 katika Sheria ya Habari na Mawasiliano Kenya Nambari 3 ya 1998 hupendekeza faini ya Sh50,000 au kifungo cha miezi mitatu jela, au adhabu zote mbili, kwa mtu anayepatikana na hatia.
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) na Mwanasheria Mkuu walikuwa wametetea sheria hiyo wakisema ililenga kulinda sifa za wengine.
Jaji Ngugi alisema maelezo ya kifungu hicho ni mapana sana na pia baadhi ya makosa yanayolengwa kwenye kifungu hicho yameangaziwa katika sheria nyingine.
Aidha, alisema hakijatimiza matakwa ya Kipengele 24 cha Sheria ambacho kinaeleza ni katika hali gani ambapo haki za kimsingi zinaweza kubanwa. Aidha, alisema kifungu hicho kinakiuka Kipengele nambari 33 cha Katiba.
“Iwapo lengo ni kulinda sifa za watu wengine, basi hilo limeangaziwa kwenye sheria ya kuwaharibia sifa watu wengine,” Jaji Ngugi alisema kwenye uamuzi wake.

Related

HABARI 4404301577424118233

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item