Mtuhumiwa wa mashambulizi ya kigaidi mjini Paris Mohamed Abrini amekiri Jumamosi (09.04.2016) kuwa mtu "aliyevalia kofia" aliyeo...

Mtuhumiwa wa mashambulizi ya kigaidi mjini Paris Mohamed Abrini amekiri Jumamosi (09.04.2016) kuwa mtu "aliyevalia kofia" aliyeonekana katika vidio pamoja na watu waliojiripua kwa kujitoa mhanga katika mjini Brussels.
Mohamed Abrini Mohamed Abrini akiwa katika kituo cha kuuzia petroli nchini Ufaransa
Mtuhumiwa wa mashambulizi ya kigaidi mjini Paris Mohamed Abrini amekiri jana Jumamosi (09.04.2016) kuwa mtu "aliyevalia kofia" aliyeonekana katika vidio pamoja na watu waliojiripua kwa kujitoa mhanga katika uwanja wa ndege wa Brussels mwezi uliopita, picha zilizoibua msako mkubwa.
Mohamed Abrini Mohamed Abrini
Abrini ameungama katika siku aliyofikishwa mahakamani akishitakiwa kwa mauaji ya kigaidi kuhusiana na mashambulizi ya mwezi Novemba mjini Paris ambapo watu 130 waliuwawa, waendesha mashitaka wamesema.
Mtuhumiwa wa ugaidi Osama Krayem , raia wa Sweden , ameshitakiwa pia kwa makosa hayo hayo kuhusiana na jukumu lake katika shambulio la kujitoa muhanga katika kituo cha treni ya mjini mjini Brussels Machi 22, ambalo lilitokea saa moja baada ya mripuko katika uwanja wa ndege. Jumla ya watu 32 walifariki katika mashambulizi hayo yaliyofuatana.
Belgien Brüssel Molenbeek Festnahme Terrorist Salah Abdeslam Salah Abdeslam wakati akimatwa mjini Brussels Machi mwaka huu
Nadharia yathibitika
Kukamatwa huko kwa watu hao kunaimarisha nadharia kwamba kundi hilo la magaidi lilifanya mashambulizi yote mawili ya kigaidi nchini Ufaransa na Ubelgiji , ambayo Dola la Kiislamu lilidai kuhusika.
Watu hao wawili ni miongoni mwa watu sita waliokamatwa katika msako mjini Brussels siku ya Ijumaa. Wawili waliachiwa huru baadaye lakini wawili wengine wameshitakiwa kwa kushiriki kwa madai ya kuwasaidia Abrini na Krayem.
Jaji anayeongoza uchunguzi nchini Ubelgiji kuhusiana na mashambulizi ya mjini Paris Novemba 13 alimfungulia mashitaka Abrini kwa kushiriki katika shughuli za kundi la kigaidi na mauaji ya kigaidi,ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu wa serikali imesema katika taarifa.
Belgien Maelbeek Metrostation in Brüssel Kituo cha chini ya ardhi cha Maelbeek mjini Brussels
Abrini Mbelgiji mwenye asili ya Morocco alikuwa mtu wa mwisho mshukiwa wa mashambulizi ya mjini Paris. Alionekana katika kamera za CCTV katika kituo cha kuuzia mafuta ya petroli kaskazini ya Paris siku mbili kabla ya mashambulizi mjini humo.
Katika gari pamoja nae alikuwa mshukiwa mwenzake wa shambulizi la mjini Paris Salah Abdeslam, ambaye anasubiri kurejeshwa kutoka Ubelgiji kwenda Ufaransa.
Waendesha mashitaka pia wamethibitisha kuhusika kwa Abrini katika mashambulizi ya uwanja wa ndege wa Brussels.
Abrini mwenye umri wa miaka 31, alikiri kuwapo katika eneo la tukio, wakati alipoonesha ushahidi, ikiwa ni pamoja na video ya mtu asiyetambulika aliyevalia kofia na jaketi la rangi ambayo haukukoza sana akionekana karibu na washambuliaji wa kujitoa muhanga wakati wakitembea katika ukumbi ambao wasafiri husubiri safari wakisukuma toroli lililokuwa na mfuko uliojaa miripuko.
Belgien Place de la Bourse Brüssel Wakaazi wa mji wa Brussels wakiandika ujumbe katika eneo la tukio la kigaidi
Washambuliaji wawili katika uwanja huo wa ndege wametambuliwa kuwa ni El Bakraoui na Najim Laachraoui, wanaoaminika kuwa watengenezaji wa mabomu katika kundi hilo.
Ni mtoto wa mkimbizi
Kaka wa Ibrahim Khalid alijiripua katika kituo cha treni cha chini ya ardhini cha Maalbeek karibu na makao makuu ya Umoja wa Ulaya mjini Brussels.
Krayem , mtoto wa mkimbizi kutoka Syria , ametanbuliwa kuwa mtu anayeonekana pamoja na Khalid muda mfupi kabla ya shambulio katika kituo hicho cha treni, wamesema waendesha mashitaka.
Krayem pia alionekana katika kamera akinunua mifuko iliyotumiwa kuvicha mabomu yaliyoripuriwa katika uwanja wa ndege, wameongeza.
Belgien Frankreich Web-Video Foto von Najim Laachraoui alias Soufiane Kayal Picha ya mshambuliaji wa kujitoa muhanga Najim Laachraoui
Vyombo vya habari vya Sweden vimesema Krayem , mwenye umri wa miaka 23 , ambaye alikulia katika mji wa kusini wa Malmo, na kuchapisha picha za mtu huyo akiwa ameshikilia bunduki ya Kalashnikov mbe ya bendera ya IS ambayo inasemekana ilichukuliwa nchini Syria.
Mtu mmoja aliyekamatwa siku ya Ijumaa na kutambuliwa kuwa ni raia wa Rwanda mwenye umri wa miaka 25 Herve B.M. anatuhumiwa kutoa msaada, kwa Abrini na Krayem, waendesha mashitaka wamesema katika taarifa.
CHANZO,DW SWAHILI

Related

MATUKIO 4434065857361154030

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item