Nyota wa Cameroon kupigania tuzo ya BBC
Enganamouit alichezea Cameroon Kombe la Dunia mwaka jana Mchezaji wa Cameroon Gaelle Enganamo...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/04/nyota-wa-cameroon-kupigania-tuzo-ya-bbc.html
Enganamouit alichezea Cameroon Kombe la Dunia mwaka jana
Mchezaji wa
Cameroon Gaelle Enganamouit ameorodheshwa kushindania tuzo ya BBC
inayotolewa kwa mchezaji bora wa kike wa mwaka 2016.
Enganamouit,
huchezea klabu ya Sweden ya Eskilstuna United, na alikuwa kwenye timu ya
Cameroon iliyofika hatua ya 16 bora katika Kombe la Dunia la Wanawake
mwaka jana.Cameroon iliondolewa na China.
Wanaoshindania tuzo:

- Gaelle Enganamouit (Cameroon, fowadi, 23)
- Amandine Henry (Ufaransa, Kiungo wa kati, 26)
- Kim Little (Scotland, Kiungo wa kati, 25)
- Carli Lloyd (Marekani, Kiungo wa kati, 33)
- Becky Sauerbrunn (Marekani, Beki, 30)
Tuma 1 kupigia Gaelle Enganamouit, 2 kupigia Amandine Henry, 3 kupigia Kim Little, 4 kupigia Carli Lloyd au 5 kupigia Becky Sauerbrunn.
Ada za kawaida za kutuma ujumbe kimataifa zitatozwa. Tafadhali, thibitisha kwanza na kampuni inayokupa huduma ya simu. Kila namba ya simu inaruhusiwa kupiga kura mara moja pekee.
Mshindi atatangazwa kupitia kituo cha redio cha BBC World Service ana mtandaoni katika bbc.com/womensfootball mnamo Jumanne 24 Mei.