PATASHIKA LEO NGUO KUCHANIKA NEW YORK
Wagombea waliobaki kwenye kinyanganyiro cha kuwania urais nchini Marekani, wanang'ang'ania kura muhimu zaidi za mchujo hii l...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/04/patashika-leo-nguo-kuchanika-new-york.html
Wagombea waliobaki kwenye
kinyanganyiro cha kuwania urais nchini Marekani, wanang'ang'ania kura
muhimu zaidi za mchujo hii leo katika jimbo la New york. Likiwa moja ya
majimbo makubwa nchini Marekania lina ushawishi mkubwa kwa wagombea
wote
.
Kwa wagombea wa chama cha Democtrats Bernie Sanders
amelelewa mjini New York naye Hillary Clinton amekuwa seneta katika
jimbo hilo.Kwa upande wa Republican mgombea mkuu Donald Trump ni mwenyeji wa jimbo hilo.
Ananuia kupata ushindi dhidi ya mshindani wake mkuu Ted Cruz, Lakini amekosoa mbinu ya kumchagua mgombea wa chama.
Mshindani wake mkuu Ted Cruz hatarajiwi kufanya vyema baada ya kukosoa sera za Trump mapema kwenye kampeni.