Raia wa Burundi waendelea kulitoroka taifa lao

Kambi ya Nyarugusu Takriban watu 260,000 wamelitoroka taifa la Burundi tangu kuzuka kwa mgogoro mwaka mmoja uliopita,huku idadi hiyo ...

Kambi ya Nyarugusu
Takriban watu 260,000 wamelitoroka taifa la Burundi tangu kuzuka kwa mgogoro mwaka mmoja uliopita,huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka hadi 330,000 kufikia mwisho wa mwaka ,iwapo suluhu ya kisiasa haitapatikana na ishara za kuzuka kwa vita vya wenyewenye kwa wenyewe kutositishwa.
Kulingana na tume ya wakimbizi katika shirika la umoja wa Mataifa UNHCR wengi wa wakimbizi waliotorokea katika mataifa jirani wamelalamikia unyanyasaji ,wa kingono kukamatwa mara kwa mara,vitisho,kuajiriwa kujiunga na jeshi na mauaji.
Tanzania ina idadi kubwa ya wakimbizi wakiwemo raia 30 wa Burundi wanaoingia nchini humo kila siku na kambi ya Nyarugusu ni miongoni mwa kambi kubwa duniani ikiwa na wakimbizi 140,540.
Tume hiyo imesema kuwa idadi nyengine ya wakimbizi katika mataifa mengine ni kama ifuatavyo:
Rwanda (76,404)
DRC (22,204)
Uganda (24,583).

Related

MATUKIO 748943883797589459

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item