Safari ya Simba Kombe la FA imemalizika leo dhidi ya Coastal Union

Baada ya michezo mitatu ya Kombe la FA kuchezwa na kushuhudia timu za Dar es Salaam Young Africans , Mwadui FC  na  Azam FC kutinga hatua ...

Baada ya michezo mitatu ya Kombe la FA kuchezwa na kushuhudia timu za Dar es Salaam Young Africans, Mwadui FC na Azam FC kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA, April 11 2016 ilikuwa zamu ya wekundu wa Msimbazi Simba kucheza mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya klabu ya Coastal Union ya Tanga.

Simba ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo wa nusu fainali dhidi ya Coastal Union kutokana na timu hiyo kuaminika kuwa chini ya kiwango na Simba kuutawala mchezo, wamekubali kipigo cha goli 2-1 wakiwa katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
DSC_0041
Coastal Union ndio walikuwa wa kwanza kupata goli la uongozi dakika ya 20 na Youssouf Sabo aliyefunga kwa mpira wa faulo. Simba walifanya mabadiliko na kumuingiza Hamis Kiiza ambaye alifunga goli la kusawazisha dakika ya 50 na kuufanya mchezo kuwa sare hadi dakika ya 85 Youssouf Sabo akapachika goli la pili kwa mkwaju wa penati iliyotokana na makosa na Novat Lufungo kumchezea faulo Shiboli.

Related

MICHEZO 3300824793165894125

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item