Unakumbuka alichokifanya Rais Magufuli sherehe za Uhuru? leo katangaza kingine

Miongoni mwa vitu vikubwa vilivyomuweka kwenye hea...


Miongoni mwa vitu vikubwa vilivyomuweka kwenye headlines Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli toka aingie madarakani ni pamoja na kutangaza kusitisha shamrashamra za sherehe za uhuru na shilingi bilioni nne iliyokua itumike kwenye sherehe hizo kitaifa ikapelekwa kwenda kutengeza barabara.

Sasa leo habari mpya ni kwamba Rais Magufuli ameahirisha shamrashamra za maadhimisho ya siku ya Muungano kwa mwaka huu ambayo huadhimishwa kila tarehe 26 ya Mwezi Aprili na badala yake ameelekeza kuwa siku hiyo itakuwa ya mapumziko kama kawaida na watanzania waiadhimishe wakiwa majumbani kwao ama katika shughuli zao binafsi.

Kufuatia kuahirishwa kwa shamrashamra hizo, Rais Magufuli ameelekeza kuwa fedha zilizopangwa kutumika kwa ajili ya kugharamia vinywaji, vyakula, gwaride, halaiki, burudani mbalimbali na hafla ya usiku ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 2, zitumike kuanzisha upanuzi wa barabara ya “Mwanza – Airport” katika eneo linaloanzia Ghana Quaters hadi Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
Barabara hiyo inafanyiwa upanuzi ili kukabiliana na kero ya msongamano mkubwa wa magari ambao unaathiri shughuli za kila siku za wananchi

Related

HABARI 86657001982541908

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item