WATU KADHAA WAUWAO KABUL
Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani anasema kuwa watu kadha wameuawa au kujeruhiwa kufuatia shambulizi la kujitoa mhanga wakati wa shug...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/04/watu-kadhaa-wauwao-kabul.html
Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani
anasema kuwa watu kadha wameuawa au kujeruhiwa kufuatia shambulizi la
kujitoa mhanga wakati wa shughuli nyingi kwenye mji mkuu wa Afghanistan
Kabul.
Walioshuhudia walisema kuwa watu kadha waliokuwa
wamejihami, waliingia kwenye majengo yaliyo karibu na makao ya shirika
la ujasusi la nchiBaada ya kutokea kwa mlipuko, milio ya risasi ilisikika. Msemaji wa wizara ya ndani amesema kuwa eneo hilo limefungwa na vikosi vya usalama.
Taliban walitangaza kutekeleza shambulizi hilo. Wiki iliyopita Taliban walitangaza kuwa wangeanzisha mashambulizi kote nchini Afghanistan.