Watumishi hewa wamponza mkuu wa mkoa Tanzania

Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga kutokana na kuwepo kwa watumishi hewa. Bi Anna ...


Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga kutokana na kuwepo kwa watumishi hewa.

Bi Anna Kilango Malecela alitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hakuwa na watumishi hewa.

Ikulu hata hivyo ilifanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza.
Awamu ya pili ya uchunguzi huo bado inaendelea katika wilaya mbili za Ushetu na Shinyanga Vijijini.
Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema amesikitishwa na hali hiyo na kuagiza mkuu huyo wa mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa Abdul Rashid Dachi kuondolewa kazini mara moja.
"Na wale wote wa Shinyanga ambao walisemekana ni zero, hakuna mtumishi hewa, walikuwa tayari wameshalipwa shilingi milioni 339.9, nimejiuliza sana, na nikajiuliza sana na kwa kweli nimejiuliza sana na kwa masikitiko makubwa, kwa nini mkuu wa mkoa alisema hakuna mtumishi hewa?" amesema Dkt Magufuli.

Kwa jumla, zaidi ya wafanyakazi hewa 2,000 waligunduliwa baada ya utathmini kufanywa mikoani

Related

HABARI 2716576733937724508

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item