Chelsea dhidi ya Tottenham
Chelsea dhidi ya Tottenham Chelsea na Tottenham wamepigwa faini kutokana na mashtaka matatu ya kushindwa kuwadhibiti wachezaji wao k...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/05/chelsea-dhidi-ya-tottenham.html
![]() |
Chelsea dhidi ya Tottenham |
Chelsea na Tottenham wamepigwa faini
kutokana na mashtaka matatu ya kushindwa kuwadhibiti wachezaji wao
katika sare ya 2-2 katika uwanja wa Stamford Bridge.
Spurs wamepigwa faini ya pauni 225,000 ikiwa ni kisa chao cha tatu kutokea.Mechi hiyo ilikuwa na kadi 12 za manjano .
Mapema mwezi huu mchezaji wa Spurs Mousa Dembele alipigwa marufuku kwa mechi sita kutokana na ghasia katika mechi hiyo hiyo ambayo ambayo ilimaliza matumaini ya Tottenham kushinda ligi ya Uingereza.
Kiungo wa kati wa Ubelgiji Dembele mwenye umri wa miaka 28 alionekana akimgusa jicho mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa.
Mkufunzi wa Tottenham Mauricio Pochettino aliingia uwanjani ili kuwatawanya mlinzi wa Spurs Danny Rose na mshambuliaji wa Chelsea Willian na mwisho wa mechi, Rose alihusika tena na makabiliano yaliomuhusisha kocha wa Blues ambaye alisukumwa na kuanguka sakafuni.