China yagundua teknolojia mpya itakayorahisisha usafiri

Wakati serikali ya Tanzania ikipambana kupunguza tatizo la usafiri na msongamano wa foleni kwa wananchi wake, Wachina wameanza kugundua te...

Wakati serikali ya Tanzania ikipambana kupunguza tatizo la usafiri na msongamano wa foleni kwa wananchi wake, Wachina wameanza kugundua teknolojia mpya ya usafiri ambayo itasaidia kupunguza foleni barabarani.
BASI
Teknolojia hiyo mpya ya usafiri haitaathiriwa na foleni za barabarani ambayo yatakuwa ni mabasi mapana ambayo kwa chini yanaruhusu magari kupita na kupishana bila wasiwasi wowote, huku yenyewe yakisafiri bila kulazimika kusimama kusubiri magari yapite, isipokuwa kwenye njia panda na kwenye taa za barabarani pekee.

Aidha basi hilo litakuwa na uwezo wa kubeba watu 1,200 kwa mara moja. Linatajwa kuwa ufumbuzi wa msongamano wa magari barabarani. Pia, lilifanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza wiki iliyopita huku magari mengine madogo yenye urefu wa futi 6.6 yanapita chini ya gari hilo jambo ambalo linaelezwa hupunguza idadi ya magari kwenye msongamano. Basi hilo linalotumia umeme na inaelezwa kwamba, linaweza kusafiri kilomita 60 kwa saa moja.

Shenzhen Hashi ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya China TBS Limited iliyohusika kutengeneza magari hayo amesema wametumia kiasi cha dola 74.1 kutengeneza basi hilo moja ambalo utengenezaji wake ulianza tangu mwaka 2010.

Related

HABARI 3040578512016674202

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item