Madaktari wapandikiza viungo vya wenye Ukimwi

Kuna uhaba mkubwa wa viungo vya kupandikizwa Madaktari nchini Uingereza wamefanikiwa kwa mara ya kwanza kupandikiza v...

Kuna uhaba mkubwa wa viungo vya kupandikizwa
Madaktari nchini Uingereza wamefanikiwa kwa mara ya kwanza kupandikiza viungo vya watu wanaougua Ukimwi kwenye wagonjwa wanaougua Ukimwi.
Kwa jumla, figo mbili na maini mawili vilipandikizwa kwa watu waliokuwa wameathirika sana na Ukimwi.
Viungo vilitolewa kwa watu baada yao kufariki.
Wataaamu wanasema mafanikio hayo yatasaidia kupunguza uhaba wa watu wanaoweza kutoa viungo na wanatumai kwamba watu zaidi wanaougua Ukimwi watajitokeza kutoa viungo vyao.
Kwa jumla, nchini Uingereza, watu watatu hufariki kila siku wakisubiri kupata viungo vya kupandikiziwa.
Ingawa kwa sasa viungo vya watu wenye Ukimwi vinaweza tu kutolewa kwa watu wanaougua Ukimwi, mtaalamu wa upandikizaji Prof John Forsythe anasema hilo bado litasaidia kwa sababu litawezesha kufanyika kwa upandikizaji katika hali ambazo awali haingewezekana.
Upandikizaji wa kwanza wa figo kwa watu wanaougua Ukimwi ulifanyika katika hospitali za Guy na St Thomas' Hospital jijini London mwaka 2015.

Related

MAAJABU 3333837664085604101

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item