Miili ya waliotoweka miaka 16 iliyopita yapatikana

Alex (kushoto) akiwa na Anker Miili ya wakwea milima wawili kutoka Marekani waliotoweka katika milima ya Himalaya miaka 16 iliyo...



Alex (kushoto) akiwa na Anker
Miili ya wakwea milima wawili kutoka Marekani waliotoweka katika milima ya Himalaya miaka 16 iliyopita imepatikana.
Mkwea milima maarufu duniani Alex Lowe alikuwa akikwea katika kilele cha Shishapangma chenye urefu wa 8,013m (26,290ft) eneo la Tibet Oktoba 1999 akiwa na mpiga picha David Bridges mkasa ulipotokea.
Wawili hao walifukiwa na maporomoko ya theluji.
Miili yao ilionekana na wakwea milima wawili wiki iliyopita ikiwa bado imekwama kwenye theluji.
Lowe alikuwa mkwea milima stadi

Image copyright ALEX LOWE FOUNDATION
Image caption Lowe alikuwa mkwea milima stadi
Bw Lowe, 40, alitambuliwa kama mmoja wa wakwea milima stadi zaidi wa kizazi chake na aliokoa wakwea milima wengi sana milimani.
Yeye na Bridges, 29, walikuwa marafiki wakuu na walikuwa wakitafuta njia mpya ya kukwea mlima Shishapangma , mlima wa 14 kwa urefu duniani.
Mkewe Lowe, Jennifer Lowe-Anker, amesema kupatikana kwa mwili wa mumewe kutasaidia familia yake kutulia.
Jennifer baadaye aliolewa na Conrad Anker mwaka 2001.


Image copyright ALEX LOWE FOUNDATION
Anker alikuwa na wakwea milima hao wawili wakati wa mkasa lakini alinusurika akiwa na majeraha madogo.
Baadaye, yeye na wenzake wengine walitafuta wawili hao kwa siku nyingi bila mafanikio.

Related

MAAJABU 6244293125613790234

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item