Mtoto mchanga atolewa kwenye vifusi Nairobi

Watu takriban 90 bado hawajulikani walipo Mtoto wa umri wa mwaka mmoja unusu amepatikana akiwa hai kwenye vifusi vya je...

Watu takriban 90 bado hawajulikani walipo
Mtoto wa umri wa mwaka mmoja unusu amepatikana akiwa hai kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka Ijumaa jijini Nairobi.
Jengo hilo la ghorofa sita liliporomoka katika mtaa wa Huruma baada ya mvua kubwa kunyesha.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, msichana huyo alitolewa kwenye vifusi mwendo wa saa kumi usiku na kukimbizwa hospitalini.
Kamanda wa kitengo cha taifa cha kudhibiti majanga Pius Maasai anasema hali ya mtoto huyo ni thabiti, kwa mujibu wa gazeti hilo.
Watu 22 wamethibitishwa kufariki na wengine karibu 90 hawajulikani walipo.
Juhudi za uokoaji bado zinaendelea siku ya nne baada ya mkasa huo kutokea.
Kufikia sasa, watu 136 wameokolewa.
Polisi wanasema wamiliki wa jumba hilo, ambalo maafisa wa baraza la jiji wanasema halikufaa kuishi watu, wamekamatwa na wanazuiliwa na polisi.
Taarifa zinasema watafikishwa mahakamani baadaye Jumanne.

Related

HABARI 3129208546459722493

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item