Wana kijiji 5 wafariki wakitafuta maji India

Ukame nchini India wasababisha uhaba wa maji Wana kijiji watano katika eneo lililokumbwa na ukame kaskazini mwa In...

Ukame nchini India wasababisha uhaba wa maji

Wana kijiji watano katika eneo lililokumbwa na ukame kaskazini mwa India wamefariki wakijaribu kutafuta maji katika kisima kisichotumika.
Wanaume hao walifariki baada ya kuvuta gesi ilio na hewa chafu ambayo ilikuwa ndani ya kisima hicho katika jimbo la Haryana kulingana na afisa mmoja.
Eneo kubwa la India linakabiliwa na ukame mbaya ambao umewaua takriban watu 300.
Haryana na majimbo mengine wiki iliopita yalikosolewa na mahakama ya juu nchini India kwa kushindwa kutambua tatizo hilo la maji.
 
Uhaba wa maji India
Ripoti katika eneo hilo zinasema kuwa wanaume hao kutoka wilaya ya Jindi huko Haryana waliamua kujaribu kukitengeza kisima hicho ili kuweza kukabiliana na ukosefu wa maji katika eneo hilo.
Lakini naibu afisa wa polisi katika wilya hiyo Virender Singh alikana kwamba walihitaji maji ya kunywa akisema wanaume hao walitaka kukitumia kisima hicho kwa maji ya kuoga na kuosha.
''Kisima hicho kilikuwa hakijatumika kwa takriban miaka mitano hadi sita na gesi yenye sumu ilikuwa imetanda huko chini'',aliambia kituo cha habari cha AFP.

Related

MATUKIO 8670270662829158715

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item