Marehemu mwalimu aliyepigwa risasi akiwakinga wakristo wasiuawe na magaidi wa Al Shabab ametuzwa medali ya juu zaidi na rais wa Keny...
https://clemencekarani.blogspot.com/2016/03/marehemu-mwalimu-aliyepigwa-risasi.html
Marehemu mwalimu aliyepigwa risasi
akiwakinga wakristo wasiuawe na magaidi wa Al Shabab ametuzwa medali ya
juu zaidi na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Rais Kenyatta alipokuwa
akihutubia taifa alisema kuwa wale wakenya wachache wanaoonesha ujasiri
wa kukabiliana dhidi ya al shabab watatuzwa.Na hivyo akasema kuwa Mwalimu Farah ametuzwa heshima ya juu zaidi nchini Kenya ya' Order Of The Grand Warrior', kwa ujasiri wake dhidi ya magaidi.
Marehemu Salah Farah alikuwa katika basi lililokuwa likiwasafirisha abiria kutoka mji mkuu wa Nairobi kuelekea Mandera walipotekwa na wapiganaji wa Al shabab.



