Atolewa kwenye ndege kwa kuongea Kiarabu
Mwanafunzi wa chuo kikuu raia wa Iraq katika jimbo la California nchini Marekani anasema kuwa alitolewa kutoka kwenye ndege ya shirika ...
https://clemencekarani.blogspot.com/2016/04/atolewa-kwenye-ndege-kwa-kuongea-kiarabu.html
Mwanafunzi wa chuo kikuu raia wa
Iraq katika jimbo la California nchini Marekani anasema kuwa alitolewa
kutoka kwenye ndege ya shirika la ndege la Southwest baada ya kufanya
mazungumzo kwa lugha ya kiarabu.
Bw Makhzoomi anasema alikuwa akizungumza na mjomba wake kwa njia ya simu kuhusu hotuba ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.
Anasema kuwa mwanamke mmoja kwenye ndege hiyo alimkodolea macho wakati alitamka jina "Inshallah" akimaanisha Mungu akipenda.
Baada ya kutumia jina hili mfanyikazi wa shirika la Southwest alimsindikiza nje ya ndege.
Bw Makhzoomi ambaye aliingia nchini Marekani kama mkimbizi kutoka Iraq na sasa ni mwanafunzi wa chuo cha Carlifonia cha Berkeley, aliambiwa kuwa hawezi kuingia tena kwenye ndege hiyo.



