Didier Drogba kulishtaki gazeti la Dail Mail
Nyota Didier Drogba amesema atachukua hatua ya kiesheria kuhusiana na tuhuma kuwa shirika lake la hisani limetumia chini ya asilimia moja ...
https://clemencekarani.blogspot.com/2016/04/didier-drogba-kulishtaki-gazeti-la-dail.html
Nyota Didier Drogba amesema atachukua hatua ya kiesheria kuhusiana na
tuhuma kuwa shirika lake la hisani limetumia chini ya asilimia moja ya
fedha zilizochangishwa kwa ajili ya miradi muhimu
Gazeti maarufu la Uingereza la Daily Mail lilisema kuwa pauni 14,000 tu
kati ya pauni milioni 1.7 zilizotolewa na wahisani kwa wakfu wa Didier
Drogba zimetumika kuwanufaisha watoto nyumbani kwao Cote d'Ivoire.Tume ya inayoshughulika na mambo ya hisani nchini Uingereza imesema inachunguza shughuli za wakfu huo ulioanzishwa mwaka wa 2009 na aliyekuwa mchezaji huyo wa Chelsea.
Drogba mwenye umri wa miaka 38, anayechezea klabu ya Montreal Impact ya Ligi Kuu ya Kandanda ya Canada, amekanusha tuhuma hizo katika taarifa yenye maneno mazito ambayo amesema habari hizo za Daily Mail ni za kumchafulia jina.


