Hospitali ya Kenya kuwatibu bure wagonjwa wa Uganda

Mashine ya kutibu ugonjwa wa saratani ilioharibika Hospitali moja nchini Kenya imeahidi kuwalipia matibabu wagonjwa w...

Mashine ya kutibu ugonjwa wa saratani ilioharibika
Hospitali moja nchini Kenya imeahidi kuwalipia matibabu wagonjwa wa saratani kutoka nchini Uganda kufuatia kuharibika kwa mashine inayotibu ugonjwa huo nchini Uganda.
Hospitali ya chuo kikuu Aga Khan imesema katika taarifa kwamba inaweza kutibu idadi ndogo ya wale wanaohitaji uuguzi.

Serikali ya Uganda tayari ilikuwa imetangaza kuwa itawasafirisha wagonjwa hao kupata matibabu nchini Kenya.
Kuharibika kwa mashine hiyo nchini Uganda kumewawacha maelfu ya wagonjwa katika hatari ya kukosa tiba.

Serikali ya Uganda imesema kuwa itagharamikia nauli ya usafiri pamoja na gharama nyengine kwa wagonjwa 400 wanaoelekea katika hospitali hiyo ya Nairobi.
Hospitali hiyo ya kibinafasi ina vitengo viwili vya kutibu saratani pamoja na madaktari sita wanaotibu ugonjwa huo

Tiba ya saratani inaweza kuwa ghali na wagonjwa wengi nchini Uganda haawezi kulipia matibabu yake.

Related

HABARI 4668840324512487672

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item