Klitschko vs Fury sehemu ya pili
Bingwa wa zamani duniani wa heavyweight bondia Vladmir Kiltschko ameelezea matumaini kuwa atayanyakua tena mataji aliyopoteza kwa Mui...
https://clemencekarani.blogspot.com/2016/04/klitschko-vs-fury-sehemu-ya-pili.html
Bingwa wa zamani duniani wa heavyweight bondia Vladmir Kiltschko
ameelezea matumaini kuwa atayanyakua tena mataji aliyopoteza kwa
Muingereza Tyson Fury wakati watakutana katika pigano la marudiano mwezi
Julai.
Akizungumza mjini Cologne, hapa Ujerumani, Klitschko alisema pigano hilo
litavutia kuanzia kengele ya kwanza hadi mwisho wake. "Yapo mengi ya
kujifunza hivyo haupaswi kuacha. Hata na miaka 40, unaendelea kujifunza
na kitu kinatokea ambacho sikuwa nimekipangia, kusimama hapa bila
mikanda. Hivyo basi natamani sana kupambana tena mara ya pili. Tunaweza
kusema mengi na kuwafurahisha watu lakini nasubiri mchuano wetu na ni
kitu ambacho kinanisisimua sana na wewe pia".Bingwa huyo wa zamani mzaliwa wa Ukraine, wa mataji ya IBF, WBA na WBO, ametumia haki yake ya kuomba pigano la pili na Fury, aliyemzidi nguvu kupitia wingi wa pointi mjini Duesseldorf Novemba mwaka jana. Fury alisema ndoto zake tangu alipokuwa mtoto, zilikuwa ni kuwa bingwa wa heavyweight. "Vladimir sio bondia wa kujituma. Hapendi kujiingiza katika hatari yoyote hivyo huenda akazungumzia mchuano mzuri anaotaka kujaribu kupigana lakini sijawahi kumwona akifanya hivyo katika mapigano yake yote. Pigano pekee la kuburudisha alilowahi kuwa nalo ni wakati alishindwa kwa njia ya knock out. Hicho ndio kinachofanyika wakati akijaribu kupigana. Kwa hivyo namsubiri sana.
Fury atapanda ulingoni na dhidi ya Klitschko mjini Manchester mnamo Julai 9.


