Machar afuta mpango wa kurejea Juba
Riek Machar Serikali ya Sudan Kusini imesema kuwa kiongozi wa waasi Riek Machar, amefutilia mbali mpango wake wa kurejea Juba kwa mu...
https://clemencekarani.blogspot.com/2016/04/machar-afuta-mpango-wa-kurejea-juba.html
![]() |
| Riek Machar |
Serikali ya Sudan Kusini imesema
kuwa kiongozi wa waasi Riek Machar, amefutilia mbali mpango wake wa
kurejea Juba kwa muda usiojulikana.
Msemaji wa serikali Michael
Makuei amesema kuwa makamu wa bwana Machar, alitaka kurejea Juba na
silaha nzito nzito, zikiwemo, magari ya kivita, makombora na bunduki
nzito nzito.Aidha amesema kuwa serikali ya nchi hiyo tayari imeruhusu wanajeshi elfu moja mia tatu na sabini kati ya elfu moja mia nne na kumi kurejea Juba kuja kumlinda Bwana Machar.
Amesema kuwa utawala wa nchi hiyo hautaruhsu wanajeshi zaidi kurejeshwa Juba, kutokana na sababu za kiusalama.
Kiongozi huyo alitoroka Juba mwaka wa 2013 baada ya rais wa nchi hiyo Salva Kirr kumtuhumu kuongoza jaribio la mapinduzi ya serikali.




