Misri: Waziri afungwa miaka 10 kwa ufisadi
Mahakama moja nchini Misri imemhukumu waziri wa zamani wa kilimo miaka 10 gerezani kwa kushiriki ufisadi. Aliyekuwa Waziri wa kil...
https://clemencekarani.blogspot.com/2016/04/misri-waziri-afungwa-miaka-10-kwa.html
Mahakama moja nchini Misri imemhukumu waziri wa zamani wa kilimo miaka 10 gerezani kwa kushiriki ufisadi.
Aliyekuwa
Waziri wa kilimo bwana Salah Helal na msaidizi wake watatumikia miaka
10 gerezani kwa kupanga njama ya kuuza kipande cha ardhi cha umma kwa
mfanyibiashara mmoja kwa bei ya chini mno.Aidha wawili hao walipigwa faini kubwa kufuatia upande wa mashtaka kupata ushahidi wa mfanyibiashara husika.
Waziri huyo wa zamani alikamatwa muda mchache tu baada ya kujiuzulu mnamo mwezi Septemba mwaka uliopita.
Mfanyibiashara huyo na mpatanishi wake walisamehewa kifungo baada ya kukubaliana na mahakama kutoa ushahidi dhidi ya waziri.




