Mkutano wa dharura waitishwa Sudan Kusini
Kamati ya pamoja inayosimamia mpango wa Amani nchini Sudan Kusini imeitisha mkutano wa dharura kujadili switafahamu inayokumba ku...
https://clemencekarani.blogspot.com/2016/04/mkutano-wa-dharura-waitishwa-sudan.html
Kamati ya pamoja inayosimamia mpango
wa Amani nchini Sudan Kusini imeitisha mkutano wa dharura kujadili
switafahamu inayokumba kurejea kwa kiongozi wa waasi Riek Machar jijini
Juba.
Mwenyekiti wa kamati Festus Mugae amesema mkataba wa amani
uko hatarini kufuatia hali hiyo. Nayo wizara ya maswali ya kigeni ya
Marekani pia imeeleza kusikitika kwake na Machar, huku ikidai Machar
anachelea kufika Sudan kimakusudi.Joto la kidiplomasia linazidi kupanda kufuatia uamuzi wa Riek Machar kutofika Juba kwa siku ya pili mfululizo.
Msemaji wa wizara ya maswali ya kigeni wa Marekani John Kirby amesema kuchelewa kwa Machar ni makusudi na inahatarisha maisha ya wananchi wa Sudan Kusini.
Aidha kamati ya kusimamia mkataba wa Amani nchini humo pia imeeleza masikitiko yake dhidi ya Machar, lakini vilevile ikaipa changamoto serikali ya Sudan Kusini kulegeza kamba ili kumwezesha Machar kurejea.
Lakini serikali ilijibu kuwa Machar alitaka kuingia nchini na idadi isiyokubalika ya wanajeshi na silaha nzito.
Msemaji wa Machar Mabior Garang alisema serikali inadanganya, na kuashiria kuwa Riek Machar atawasili Juba hii leo kusipokuwa na hitilafu.
Kurejea kwa Machar ni hatua muhimu ya kutekeleza mkataba wa amani uliotiwa sahihi mwezi Agosti mwaka jana.
Iwapo atarejea, ataapishwa kama makamu wa rais , kisha kutakiwa kuunda serikali ya muungano na rais Salva Kiir
Riek Machar aliiaga Sudan Kusini mnamo mwaka wa 2013 vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipoanza.
Tangu hapo maelfu ya watu wameuawa, huku zaidi ya watu milioni mbili wakipoteza makao.





