Mwanamuziki mashuhuri wa Congo Papa Wemba afariki dunia

Papa Wemba mmojawapo wa wanamuziki mashuhuri kabisa barani Afrika amefariki mapema Jumapili (24.04.2016) nchini Ivory Coast. Papa We...


Papa Wemba mmojawapo wa wanamuziki mashuhuri kabisa barani Afrika amefariki mapema Jumapili (24.04.2016) nchini Ivory Coast.
Papa Wemba katika mojawapo ya matumbuizo yake. Papa Wemba katika mojawapo ya matumbuizo yake.

Kwa mujibu wa mtandao wa lebabi.net iliowanukuu waandalizi wa tamasha la muziki lililokuwa likifanyika katika mji mkuu wa Abidjan ,Wemba mwenye umri wa miaka 66 alianza kujisikia vibaya wakati alipokuwa jukwaani kuonyesha muziki wake.

Gazeti la Ufaransa Le Monde limesema Papa Wemba alizirai wakati akiwa katika jukwaa.
Mwanamuziki huyo ambaye jina lake la kuzaliwa lilikuwa Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba maisha yake ya muziki yamedumu takriban kwa miongo mitano.Ana umashuhuri mkubwa barani Afrika na pia duniani kwa jumla kutokana na ushirikiano wake na Peter Gabriel.
Miongoni mwa nyimbo zake zilizotia fora ni pamoja na Sai Sai,Yolele na Maria Valencia.

Related

BURUDANI 6999380024842963734

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item