TCRA imethibitisha kupungua kwa idadi ya simu feki nchini.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango zimeendelea kupungua kutoka asil...

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango zimeendelea kupungua kutoka asilimia 30 mwezi Desemba hadi kufikia asilimia 13, Machi mwaka huu. Kutokana na kupungua huko, inamaanisha kwamba simu feki nchini zinazidi kupungua.
Akizungumza na vyombo vya habari jana, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA James Kiraba amesema katika uchambuzi na matokeo ya awali ambacho pia kilishirikisha kampuni za mawasiliano kimeonyesha kuwa mwezi Februari ilishuka mpaka asilimia 18.

Amesema uchambuzi wa Februari ulionyesha idadi ya namba tambulishi ambazo hazikuwa na viwango zilikuwa asilimia tatu, vilevile idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa na asilimia 18, huku simu halisi zikiwa asilimia 79.

“Uchambuzi wa Machi unaonyesha idadi ya namba tambulishi ambazo hazina viwango zilikuwa sawa na asilimia mme, huku idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa asilimia 13. Uchambuzi huu unahusisha kampuni zote za simu nchini,” amesema Kiraba.

Related

HABARI 2458591660977538343

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item