Ugomvi wa kikombe cha chai wasababisha maafa Misri

Maandamano ya hasira nchini Misri Kumekuwa na maandamano ya hasira yaliofanywa na mamia ya watu mjini Cairo baada ya m...

Maandamano ya hasira nchini Misri
Kumekuwa na maandamano ya hasira yaliofanywa na mamia ya watu mjini Cairo baada ya maafisa wa polisi kumpiga risasi na kumuua mchuuzi mmoja kuhusu kile walioshuhudia wanasema ni bei ya kikombe kimoja cha chai.
Mtu mmoja zaidi alipigwa risasi na kujeruhiwa katika kisa hicho kilichofanyika mashariki mwa makaazi ya mji mkuu wa taifa hilo.
Afisa mmoja mwanadamizi katika kikosi cha polisi amesema kuwa mgogoro huo ulikuwa ni kuhusu bei ya kikombe cha chai.
Kanda za video zimechapishwa mtandaoni zikionyesha uma wa watu ukivunja gari moja la maafisa wa polisi huku ukisema kuwa ''polisi na majambazi''.
Kumekuwa na msururu wa madai ya ukatili unaodaiwa kutekelezwa na polisi katika miezi ya hivi karibuni ambao umesababisha maandamano ya hasira.

Related

HABARI 8770532036938069129

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item