Ukraine yaadhimisha miaka 30 ya janga la Chernobyl

Chernobyl Ukraine inaadhimisha miaka 30 ya kumbukumbu za janga la kinu cha kinyuklia la Chernobyl. ...

Chernobyl

Ukraine inaadhimisha miaka 30 ya kumbukumbu za janga la kinu cha kinyuklia la Chernobyl.
Ving'ora vilisikika kwa wakati mmoja na mda uliofanyika mlipuko wa kinu hicho mapema mnamo tarehe 26 mwezi Aprili mwaka 1986.
M'momonyoko katika kinu hicho unasalia kuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea katika historia.
Paa lililipuka na moshi mkubwa wa vifaa vya radioactive kutapakaa kila mahali, na kusambaa kote katika mipaka ya Ukraine, hadi nchi jirani ya Belarus na kaskazini mwa bara Ulaya.
Jamaa za wale waliofariki katika mkasa huo walishiriki katika maadhimisho hayo makanisani kwa kuwasha mishumaa na kukesha usiku.
Wafanyikazi 31 wa kinu hicho cha kinuklia pamoja na wafanyikazi wa shirika la zima moto walikuwa baadhi ya watu wa kwanza kufariki katika mkasa huo, ilihali maelfu ya wengine walikufa kutokana na athari ya miale ya nuklea na maradhi yanayohusishwa na janga hilo baya.
Idadi kamili ya wale wote waliofariki katika mkasa huo bado haijatolewa

Related

MATUKIO 7126930695687249605

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item