Wakenya waliofikishwa ICC wafurahia uhuru

Wakenya sita waliokuwa wamefunguliwa mashtaka na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) kuhusiana na ghasia za baada ya uc...


Wakenya sita waliokuwa wamefunguliwa mashtaka na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 wamekusanyika kwa mkutano wa maombi mjini Nakuru kusherehekea kutamatishwa kwa kesi dhidi ya Naibu Rais William Ruto na mwanahabari Joshua Sang.
Mji wa Nakuru unapatikana katika uliokuwa mkoa wa Bonde la Ufa na uliathirika sana wakati wa mapigano hayo.
Rais Uhuru Kenyatta, aliyekuwa miongoni mwa waliofunguliwa mashtaka, amekuwa akihimiza maridhiano na umoja.
Wengine waliokuwa wamefunguliwa mashtaka ni aliyekuwa mkuu wa polisi Meja Jenerali Hussein Ali, aliyekuwa mkuu wa utumishi wa umma Francis Muthaura na waziri wa zamani Henry Kosgey.
Watu takriban 1,300 walifariki na wengine 600,000 wakafurushwa makwao, wengi wao eneo la Bonde la Ufa, wakati wa mapigano hayo.

Mahakama ya ICC awali ilithibitisha mashtaka dhidi ya Bw Kenyatta, Bw Ruto na Bw Sang lakini kesi dhidi ya Bw Kenyatta ikaondolewa Desemba mwaka 2014.
Kesi dhidi ya Bw Ruto na Bw Sang ilitamatishwa na majaji mapema mwezi huu.
Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya ICC Fatou Bensouda alikuwa amelalamika kwamba mashahidi wengi wamehongwa au kutishwa na wakabadilisha ushahidi waliokuwa wametoa awali na wengine wakajiondoa.
Wakati wa kutamatisha kesi dhidi ya Bw Ruto na Bw Sang tarehe 5 Aprili, Jaji Chile Eboe-Osuji kwenye uamuzi wake alisema huenda kuingiliwa kwa mashahidi kulidhoofisha kesi hiyo.
Aidha, alisema kulikuwa na uingiliaji wa kisiasa ambao huenda uliwatia hofu baadhi ya mash

Wiki hii, mjadala kuhusu kesi hizo umefufuliwa tena baada ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga kukosoa hatua ya ICC kutamatisha kesi dhidi ya viongozi wakuu Kenya.
Alisema hilo huenda likawafanya viongozi na wanasiasa Afrika kutozingatia mfumo wa sheria wanapotawala.

Bw Odinga alidai kwenye mahojiano na shirika la habari la AFP kwamba kutokana na uamuzi huo wa ICC, viongozi wengi wa kiafrika watakuwa madikteta na hawataogopa kushtakiwa na ICC kwa vile wanaweza kuhitilafiana na ushahidi bila kujali madhara yake.

Bw Kenyatta na Bw Ruto wakijibu madai hayo kwenye mkutano wa hadhara eneo la Nyandarua, katikati mwa Kenya, walimshutumu Bw Odinga wakisema alitaka kujifaidi kisiasa kupitia kesi hizo.
Hisia miongoni mwa Wakenya zimegawanyika baadhi wakisema kuna haki ya kusherehekea kutamatishwa kwa kesi dhidi ya Wakenya hao.
Kuna wengine hata hivyo wanaoamini kwamba si haki kusherehekea ikizingatiwa kwamba wengi wa waathiriwa wa ghasia hizo bado wanateseka.

Kwenye Twitter, mgawanyiko huo unajitokeza wazi kukiwa na vitambulisha mada vinavyoshindana.
Wanaounga mkono mkutano huo wa Afraha, Nakuru na kuhimiza maridhiano wanatumia kitambulisha mada #WeAreOneAfraha (Sisi tuna umoja Afraha) na #UhuruRutoThanksgiving (Ibada ya kutoa shukrani ya Uhuru

Related

HABARI 4570168329208721217

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item