Ndege kubwa zaidi duniani yatua Australia
Antonov An-225 Mriya ndiyo ndege refu na nzito zaidi kuwai kujengwa. Antonov An-225 Mriya ilitoka mjini Prague na kusimama maeneo ka...
https://clemencekarani.blogspot.com/2016/05/ndege-kubwa-zaidi-duniani-yatua.html
![]() |
| Antonov An-225 Mriya ndiyo ndege refu na nzito zaidi kuwai kujengwa. |
![]() |
| Antonov An-225 Mriya ilitoka mjini Prague na kusimama maeneo kadha mashariki ya kati na Asia, ikiwa safarini kwenda Australia. |
![]() |
| Ngege hii ina jumla ya magurudumu 32 na injini sita |
Maelfu ya watu nchini Australia
wanaopenda ndege walikusanyika kutizama ndege kubwa zaidi duniani ya
Antonov An-225 Mriya, ilipowasili mjini Perth nchini humo.
Misongamano ya magari ilifunga barabara wakati umati ulikusanyika kutizama kuwasili kwa ndege hiyo.
Ndege hiyo ilitoka mjini Prague na kusimama maeneo kadha mashariki ya kati na Asia, ikiwa safarini kwenda Australia.





