UEFA inaandaa mkutano mkuu Budapest
Kamati kuu ya UEFA inakutana mjini Budapest katika mkesha wa mkutano mkuu wa Shirikisho hilo la Kandanda Ulaya lakini hatima ya rais wao ...
https://clemencekarani.blogspot.com/2016/05/uefa-inaandaa-mkutano-mkuu-budapest.html
Kamati kuu ya UEFA inakutana mjini Budapest katika mkesha wa mkutano
mkuu wa Shirikisho hilo la Kandanda Ulaya lakini hatima ya rais wao
aliyesimamishwa kazi Michel Platini itaighubika mikutano hiyo
Uongozi wa UEFA utajadili leo miundo ya mashindano, masuala ya kinidhamu
na kusikiliza ripoti nyingine muda mfupi kabla ya kuanza dimba la Kombe
la Mataifa ya Ulaya Euro 2016 nchini Ufaransa kuanzia Juni 10.UEFA inataka kudhihirisha kuwa ingali na uwezo wa kufanya kazi na kuchukua maamuzi katika wakati huu ambapo kuna mgogoro wa uongozi, huku ikisubiri uamuzi wa Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro ya Michezo kuhusu Platini. Platini alikata rufaa dhidi ya hatua ya FIFA kumsimamisha kazi na kesi hiyo ikasikilizwa Ijumaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro ya Michezo.


