Ada ya kupiga simu Ulaya yashuka kwa 75%
Raia wa Ulaya wakipiga selfie Ada ya kupiga simu kupitia mitandao mingine katika muungano wa bara Ulaya imeshuka kwa kiwango kikubw...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/04/ada-ya-kupiga-simu-ulaya-yashuka-kwa-75.html
![]() |
Raia wa Ulaya wakipiga selfie |
Ada ya kupiga simu kupitia mitandao
mingine katika muungano wa bara Ulaya imeshuka kwa kiwango kikubwa,
ikiwa ni hatua ya mwisho kabla ya ada hiyo kuondolewa kabisa kwa raia wa
bara Ulaya mwaka ujao.
Ada hiyo huwa haiwapendezi raia wengi wa bara hilo wanaosafiri kwa shughuli za kibiashara na burudani.Tume ya muungano huo inasema ada hiyo imeshuka kwa asilimia 75.
![]() |
Raia wa Ulaya anayepiga simu |
Mamilioni ya Waingereza hutumia pauni milioni 350 kila mwaka kutokana na ada hizo za kupiga simu miongoni mwa mataifa ya bara hilo,alisema waziri wa uchumi wa kidijitali Ed Vaizey.