Dadake Prince ataka kurithishwa mali

Tyka Nelson Nyota wa muziki wa Pop Prince hakuwacha wasia ,dadaake amefichua katika stakhabadhi za mahakama. Nakala zilizowasilish...


Tyka Nelson
Nyota wa muziki wa Pop Prince hakuwacha wasia ,dadaake amefichua katika stakhabadhi za mahakama.
Nakala zilizowasilishwa katika mahakama ya jimbo la Minnesota zinaonyesha,Tyka Nelson ametoa ombi la mtu atakayesimamia mali ya nyota huyo.
Prince mwenye umri wa miaka 57 alipatikana amefariki katika lifti katika studio yake ndani ya makaazi ya Minneapolis,huko Minnesota Alhamisi iliopita.
Prince
Ukubwa wa mali yake haujulikani lakini unadaiwa kuwa dola milioni 27.
Nelson ni dadaake Prince aliyesalia na amesema katika nakala hizo kwamba hatua za haraka zinafaa kuchukuliwa ili kusimamia biashara za nduguye.
Nyimbo za Prince zimetewala chati za Uingereza wiki hii,huku mashabiki wanaomuomboleza wakinunua muziki wake huku ripota wa Hollywood akisema kuwa zaidi ya nyimbo milioni tatu za muziki wake pamoja na albamu zimenunuliwa nchini Marekani tangu kifo chake.

Related

MATUKIO 3670728401518792074

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item