Taifa Stars kuivaa Harambe Stars
Timu ya Taifa ya Tanzania inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya Taifa Kenya Mei 29, jijini Nairobi. Mchezo huo...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/04/taifa-stars-kuivaa-harambe-stars.html
Timu ya Taifa ya Tanzania inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya Taifa Kenya Mei 29, jijini Nairobi.
Mchezo
huo utachezwa jijini Nairobi Mei, 29 mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya
maandalizi kwa timu zote mbili kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu
kwa Fainali za Mataifa Afrika mwezi Juni, 2016 ambapo Taifa Stars
itacheza dhidi ya Misri Juni 04, mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam.TFF kwa kushirkiana na FKF zimekubaliana kuwepo kwa mchezo huo wa kirafiki, utakotumika kama sehemu za maandalizi kwa timu zote kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa AFCON 2017 mwezi Juni.
Kikosi cha Taifa Stars kinachonolewa na kocha mkuu, Charles Boniface Mkwasa kinatarajiwa kuingia kambini mwezi Mei, mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya Vodacom (VPL) kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki kabla ya kuwakabili Misri mwezi Juni, 2016.