Kamanda wa Machar awasili Juba Mkuu wa jeshi linalomuunga mkono kiongozi wa w...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/04/kamanda-wa-machar-awasili-juba-mkuu-wa.html
Mkuu wa jeshi
linalomuunga mkono kiongozi wa waasi Riek Machar, bwana Simon Gatwech
Dual amewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Juba.
Kuwasili
kwake kunaibua matumaini ya kufufuka kwa harakati za kutekelezwa
kikamilifu kwa mkataba wa amani uliotiwa sahihi yapata miezi 8
iliyopita.Kamanda huyo Gatwech Dual aliwasili kutoka Ethiopia akiandamana na kikosi cha wanajeshi 100.
Hiki kilionekana kuwa ni kikwazo kikubwa kwa kiongozi wa waasi kuweza kurejea Juba ambapo alisisitiza kuwa lazima kwanza awasili Gatwech, wanajeshi pamoja na silaha.
Msemaji wa waasi alisema Machar sasa atarejea Juba kesho
Machar, ambaye aliondoka juba wakati vita vya wenywe ka wenyewe vilipoanza Desemba mwaka wa 2013, anatarajiwa kuunda serikali ya umoja na mpinzani wake mkuu Rais Salva Kiir.

Kwa sasa, Machar yuko katika kambi ya waasi karibu na mpaka wa Ethiopia.
Itambidi avuke hadi Ethiopia, kwa uwanja wa ndege ambao uko karibu, katika maeneo ya Gambela, ili aweze kupanda ndege ya kuelekea Juba
Msemaji wa waasi William Ezekiel amenukuliwa akisema kwamba wapiganaji wa Machar wapatao 195 pamoja na mkuu wa majeshi Simon Gatwech Dual amabao wamewekwa chini ya vikwazo na Marekani na Umoja wa Mataifa, pia walikuwa wanatarajiwa kurejea Juba hii leo.
Ezekiel amelaumu kuchelewa kurejea kwa Machar mjini Juba kutokana na wahisani ambao walikuwa wanafadhili msafara wake kujiondoa.
Maelfu ya watu wameuawa na zaidi ya milioni mbili kutoroka makwao kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
![]() |
Kwa sasa, Machar yuko katika kambi ya waasi karibu na mpaka wa Ethiopia |
Ubalozi wa Uingereza unasisitiza kwamba kurejea kwa Machar ni muhimu sana katika mchakakato wa kuunda serikali ya Umoja