Obama atembelea maonyesho ya biashara Hannover
Obama atembelea maonyesho ya biashara Hannover Rais Barack Obama ametembelea maonyesho ya biashara na viwanda ya Hannover pamoja na Kans...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/04/obama-atembelea-maonyesho-ya-biashara.html
Obama atembelea maonyesho ya biashara Hannover
Rais Barack Obama ametembelea maonyesho ya biashara na viwanda ya
Hannover pamoja na Kansela Angela Merkel kabla ya kuwa na mazungumzo na
viongozi wa Ulaya juu ya masuala ya dunia na usalama.

Amesema hiyo hii ni fursa nyengine kwake kumwambia kila mtu aje hapo na kununuwa bidhaa zilizotengenezwa Marekani.
Rais Barack Obama wa Marekani akizungumza akiwa katika banda la Marekani leo hii wakati alipotembelea maonyesho hayo ya biashara na viwanda ya Hannover akiandaman na mwenyeji wake Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ambapo amesema yuko Hannover kwa sababu ana fahari kuonyesha mwamko wa ubunifu wa Marekani.
Kufunguliwa rasmi kwa maonyesho

Wakati wakianza kukaguwa mabanda ya Marekani na Ujerumani katika maonyesho hayo Kansela Angela Merkel wa Ujerumani alitamka kwa Kingereza kwa kuwa utamu wa puding ni kuila basi na waanze.
Obama na Merkel walitembelea vibanda vya Marekani vya kutengeneza mashine za kuchapisha za 3D ,vifaa vya kompyuta na teknolojia ya anga za juu wakiandamana na mkururo wa wapiga picha, waandishi wa habari, maafisa usalama na mawaziri.
Merkel ni mwanasayansi

Wakati alipokuwa katika banda moja rais huyo alifanya mzaha kwamba mara atakapokuwa hayuko tena madarakani atatafuta wakati wa kuanza kubuni vitu.
Ziara ya siku mbili ya Obama nchini Ujerumani ni kituo cha mwisho cha ziara yake ya mataifa matatu ambayo ilimfikisha Uingereza na Saudi Arabia.Ziara hii pia inakuja kabla ya kufanyika kwa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO katika mji mkuu wa Poland Warsaw.
Mkutano mdogo wa kilele
Baada ya hotuba yake kwa viongozi wa biashara Obama ataungana na Merkel kwa mazungumzo juu ya masuala yanayoikabili dunia hivi sasa ambayo pia yatahudhuriwa na Rais Francois Hollande wa Ufaransa, Waziri Mkuu wa Italia Matteo Renzi na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron.
Mazungumzo hayo ambayo yanatajwa kwa mkutano mdogo wa kilele pia yatagusia mapambano dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam nchini Syria na Iraq,mzozo wa wakimbizi barani Ulaya ,mzozo wa Libya, kura ya maoni ya Uingereza juu ya uwanachama wake wa Umoja wa Ulaya na makubaliano ya biashara kati ya Marekani na Ulaya yanayopendekezwa pamoja na hatua za kudhibiti mabavu ya Urusi.