Kenya yaitaka ICC kuikabidhi faili za washukiwa 3
Mahakama ya ICC Kenya sasa inataka faili za kesi zinazowakabili wakenya watatu wanaotuhumiwa kuingilia ushahidi wa ma...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/04/kenya-yaitaka-icc-kuikabidhi-faili-za.html
![]() |
Mahakama ya ICC |
Kenya sasa inataka faili za kesi
zinazowakabili wakenya watatu wanaotuhumiwa kuingilia ushahidi wa
mashahidi wa ICC kushtakiwa nchini humo.
Mwanasheria mkuu Profesa
Githu Muigai amesema kuwa Kenya ina mahakama zilizo na uwezo za kushtaki
kesi ndogo kufuatia kuanguka kwa kesi kuu iliowahusisha wakenya sita
maarufu kama Ocampo 6.Mwanasheria huyo pia ameshtumu idara ya mashtaka katika mahakama ya ICC kwa kushindwa kushirikiana na Kenya kuhusu ombi la awali lililowasilishwa kwa aliyekuwa kiongozi wa mashtaka Moreno Ocampo kuikabidhi Kenya faili zote za washukiwa.
Ameongezea kuwa mpango wa Kenya kujiondoa katika mahakama hiyo utaangaziwa na Umoja wa Afrika AU na kwamba Kenya kama taifa haijaanza harakati za kujiondoa.