Kanali wa jeshi auawa Burundi
Ghasia zilizokuwa nchini Burundi Kanali mmoja wa jeshi amepigwa risasi na watu wasiojulikana katika mji mkuu wa Burund...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/04/kanali-wa-jeshi-auawa-burundi.html
![]() |
Ghasia zilizokuwa nchini Burundi |
Kanali mmoja wa jeshi amepigwa
risasi na watu wasiojulikana katika mji mkuu wa Burundi
,Bujumbura,kulingana na vyombo vya habari vya kundi la SOS nchini humo.
Kanali
Emmanuel Buzubona aliuawa pamoja na mtu mmoja aliyekuwa akiendesha
pikipiki siku ya Jumatano kaskazini mwa makaazi ya mji huo.Ni miongoni mwa maafisa wa jeshi wa hivi karibuni kuuawa tangu rais Pierre Nkurunziza kunusurika jaribio la mapinduzi na maandamano kufuatia hatua yake ya mwaka jana kujiongezea mda wa kuhudumu kama rais wa taifa hilo.