Maharamia wateka meli ya Uturuki Nigeria
Maharamia katika pwani ya Nigeria wameshambulia meli ya mizigo ya Uturuki na kuwateka nyara wafanyikazi sita wa meli hiyo, katika eneo ...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/04/maharamia-wateka-meli-ya-uturuki-nigeria.html
Maharamia katika pwani ya Nigeria
wameshambulia meli ya mizigo ya Uturuki na kuwateka nyara wafanyikazi
sita wa meli hiyo, katika eneo hilo ambalo limeshuhudia visa vingi vya
uharamia miaka ya hivi karibuni.
Meli hiyo inamiikiwa na kampuni ya Kaptanogul, ambayo ililiambia shirika hilo la habari kuwa wale waliotekwa nyara pamoja na wale waliosalia melini wote wako katika hali nzuri ya afya.
Haijulikani ni wafanyikazi wangapi walikuwa ndani ya meli hiyo, ambayo ilikuwa ilikuwa ikisafirisha kemikali wakati iliposhambuliwa, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.