Ukame walazimu treni ipeleke maji kilomita 300
Gari la moshi la dharura lililobeba lita nusu milioni ya maji inatarajiwa kuwasili Magharibi mwa India kukata kiu ya wenyeji wa ...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/04/ukame-walazimu-treni-ipeleke-maji.html
Gari la moshi la dharura lililobeba
lita nusu milioni ya maji inatarajiwa kuwasili Magharibi mwa India
kukata kiu ya wenyeji wa eneo hilo lililokumbwa na ukame.
Gari la moshi hilo linaloitwa ''Treni ya maji'' linavuta mabehewa 10 makubwa yaliyojaa maji.Mabehewa 100 ya maji yatasafirishwa umbali wa kilomita 300 hadi Latur katika jimbo la Maharashtra Kusini.
Jimbo hilo linakumbwa na ukame mbaya sana katika kipindi cha karne moja iliyopita.
Ukame huo umesababisha hata hospitali katika eneo hilo la Kusini kuahirisha operesheni ya wagonjwa kwa sababu ya uhaba wa maji.