Uhuru ataka mmiliki wa jumba la maafa kukamatwa

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametaka kukamatwa kwa mmiliki wa nyumba ilioanguka mjini Nairobi na kuwaua watu saba. Kenyatta aliyezur...


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametaka kukamatwa kwa mmiliki wa nyumba ilioanguka mjini Nairobi na kuwaua watu saba.
Kenyatta aliyezuru mkasa wa tukio hilo pia amewataka wakaazi wa nyumba zilizopo karibu na eneo hilo kuondoka wa kuwa nyumba hizo zimethibitishwa kutokuwa salama.
Maafisa wa Kaunti ya Nairobi wamethbitisha kuwa nyumba hiyo ilikuwa imeorodheshwa miongoni mwa majumba yaliotarajiwa kuvunjwa kwa kuwa haikuafikia viwango vya nyumba ya kuishi watu wengi.

 
Rais Uhuru Kenyatta
Juhudi za uokoaji zinaendelea lakini zimetatizwa na mvua kubwa inayoendelea mbali na uwezo wa kufikia eneo hilo.
Jeshi la Kenya linaloongoza juhudi hizo za uokozi limelazimika kutumia mikono na misumeno ya kielektroniki kuchimba chini ya vifusi kwa kuwa vifaa vinavyohitajika katika zoezi hilo haviwezi kuingia katika eneo hilo.

Related

HABARI 4978091468637024525

Post a Comment

emo-but-icon

MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII

KILIMANJARO MOUNTAIN IN TANZANIA

http://www.tanzaniaparks.go.tz/

welcome in Tanzania at Arusha Mount meru

https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=7138641291977024838#editor/target=post;postID=3203923396230239409

https://web.facebook.com/kephasilani?fref=ts

Recent

Comments

item