ATLETICO WALIVYOKAMILIASHA MAZOEZI YA MWISHO KUIKABILI MADRID
Atletico Madrid ndiyo walikuwa wakwanza kufanya mazoezi yao ya mwisho kwenye uwanja wa San Siro kuelekea mchezo wa fainali yao ya klab...

http://clemencekarani.blogspot.com/2016/05/atletico-walivyokamiliasha-mazoezi-ya.html

Atletico Madrid ndiyo walikuwa wakwanza kufanya mazoezi yao ya mwisho kwenye uwanja wa San Siro kuelekea mchezo wa fainali yao ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.
Namna ambavyo wamefanya mazoezi yao inaashiria kabisa ni jinsi gani watacheza mchezo wao wa kesho kwa kujaza viungo wengi kwenye katikati ya uwanja.
Siri ya mafanikio ya Atletico Madrid ni kucheza pressing game, leo wakati wanafanya mazoezi yao ya mwisho walitumia sehemu ndogo ya katikati ya uwanja kwa kuukata uwanja katika eneo la mraba na kucheza pasi za haraka ndani ya eneo hilo la mraba.


Ili kuweza kushinda vita ya eneo la katikati ya uwanja, inawabidi Atletico wafanye kazi kubwa ya pressing na ku-win possession kwa haraka na kutengeneza nafasi kwa haraka.

Eneo la nje la mraba huo walikuwepo mabeki wa pembeni ambao kazi yao ilikuwa ni kulazimisha wapinzani wao ili mipira iende pembeni kwenye wings na kuwabana huko kwa haraka ili warudishe mipira kwenye himaya yao na kuweza kushambulia kwa namna wanayotaka wao.